Kampeni ya I am Beijing +25

Utangulizi
Mwaka 2020 unaweka alama muhimu ulimwenguni katika eneo la usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Mfumo madhubuti zaidi duniani juu ya usawa wa kijinsia-Mpango wa Utekelezaji wa Beijing unatimiza miaka 25 mwaka huu. 2020 pia ni mwaka wa 20 wa Azimio la 1325 la Baraza la Usalama, miaka 5 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, miaka 10 ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake (UN Women) na miaka 75 ya Umoja wa Mataifa. Maadhimisho haya yanafanyika katika muktadha wa hatua muhimu za kimataifa, kikanda na kitaifa, fursa na changamoto za maendeleo ya haki za wanawake na ajenda ya usawa wa kijinsia.

Wakati wanawake wa Kitanzania walikuwa mstari wa mbele katika kuweka na kushawishi ajenda na maudhui ya Mpango wa Utekelezaji wa Beijing kuanzia 1995, wasichana hususan wale ambao walizaliwa kuanzia mwaka 1995 hawauelewi vizuri. Kumekuwa na jitihada za kuwaleta pamoja wasichana, hata hivyo, juhudi hizo zimekuwa kama za zimamoto, zikiegemea zaidi maeneo ya mjini, zikifanywa kimila na kijadi na hivyo kushindwa kuvuta hisia za wasichana ili wawe washiriki wa harakati hizo.

Kwa kufuatilia uwajibikaji, UNWOMEN inasimamia utekelezaji wa Jukwaa la Beijing (BPfA) kila baada ya miaka mitano, yaani, Beijing +5, +10, +15 +20 na sasa Beijing +25. Uhakiki wa kikanda umeshuhudia uwasilishaji wa ripoti mbili, za serikali na ripoti za mashirika ya kiraia. Ushiriki wa wasichana wa Kitanzania ulikuwa mdogo, kwa kiasi kikubwa, kwa sababu ya kutokuwapo kwa taarifa za kutosheleza kuhusu michakato na vikwazo vya kifedha.

Kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 25 ya Mpango wa Utekelezaji wa Beijing, kuna mikutano mbalimbali ya kimataifa, kikanda na kitaifa ambayo itafanyika ndani ya mwaka 2020. Mikutano ya kimataifa itafanyika Machi, Mei, Julai na Septemba huko New York, Mexico, Paris na New York. Mikutano hiyo itatoa nafasi kwa Mazungumzo juu ya hatua za haraka na uwajibikaji katika utekelezaji wa masuala ya usawa wa kijinsia.

Kusherehekea nguvu ya harakati za haki za wanawake, mshikamano wa wanawake, na uongozi wa vijana kufikia mabadiliko. Kukabidhi kijiti cha uhamasishaji kutoka kwa Mavetereni wa Beijing 1995 kwenda kwa kizazi kipya cha wasichana na wanawake.

a. Kufanya thathmini ya mchakato na kuweka ajenda ya utekelezaji wa hatua thabiti za kutambua usawa wa kijinsia kabla ya 2030. Kwa mtazamo wa kuhakikisha wasichana wa Kitanzania wajua Mpango wa Utekelezaji wa Beijing na wanashiriki kikamilifu katika kupanga hatua za kutafuta wa usawa wa kijinsia haraka, Msichana Initiative na Her Ability Foundation wanatarajia kutekeleza kampeni ya I am Beijing + 25 (Mimi ni Beijing +25)

Wito wa Kutuma Maombi
Msichana Initiative na Her Ability Foundation kupitia Kampeni ya I am Beijing +25 tunatafuta wasichana 25 kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wenye asili, uzoefu na ujuzi tofauti kuwa mstari wa mbele katika kuelezea mustakabali wa Jukwaa la Beijing. Wasichana hao 25 pia watawaongoza na kuwahamasisha wasichana wengine,
wanajamii na serikali kuchukua hatua kuelekea kwenye utekelezaji wa ahadi za usawa wa kijinsia katika ngazi za kitaifa, ngazi za kitaifa na zaidi ya hapo.

Vigezo vya Kuchaguliwa
Awe na umri wa miaka 18 mpaka 25, mwenye shauku kubwa ya haki za wasichana na wanawake
A. Anafanya kazi ya kuendeleza haki za wasichana na wanawake katika maeneo yake

B. Wana uwezo wa kuunda, kudumisha na kupeleka maarifa kwa wasichana wengine 25 na hivyo kuwezesha kina dada 625 (Impact Sisters) kupata mafunzo ambayo yataendeleza kasi ya ushiriki wa wasichana katika kusimamia ajenda ya usawa wa kijinsia katika ngazi za chini, kitaifa Tanzania na kuhakikisha inakwenda vizuri.

C. Awe na uwezo wa kutenga muda wake kushiriki katika shughuli muhimu katika utekelezaji wa kampeni.

D. Uwezo wa kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kuendeleza mazungumzo na kushawishi mabadiliko.

E. Kuwa na uwezo wa kuandaa hafla za kitaifa katika kuainisha mipango ya kimataifa ya utekelezaji kuelekea utambuzi wa usawa wa kijinsia.

F. Nafasi 5 zitatengwa kwa ajili ya wasichana wenye ulemavu.

G. Asilimia 80 ya washiriki watakaochaguliwa, watatoka nje ya Mkoa wa dar es Salaam.

H. Uwezo mkubwa katika lugha ya Kiswahili na uwezo mkubwa katika lugha ya Kiingereza zitakuwa sifa za ziada.

Jinsi ya kuomba
Tutumie shairi, wimbo, michoro, insha au njia yoyote ya ubunifu ukijibu maswali yafuatayo.

Jielezee kwa kifupi? (Zingatia kile unachofanya katika kuendeleza haki za wasichana na wanawake katika jamii yako) (maneno yasizidi 200)

Unafahamu nini kuhusu Jukwaa la Beijing na uhusiano wake na haki za wasichana na wanawake? Beijing +25 inamaanisha kwako ukiwa msichana wa Tanzania? (maneno yasizidi 200)

Ikiwa utakubaliwa katika programu hii, utawezaje kuleta kwa pamoja, kusimamia nakuendeleza kikundi cha wasichana wengine 25 kama Dada wenye Kuleta Matokeo ya Beijing? (maneno yasizidi 200)

Maelekezo:
Maombi yote yatumwa kwa barua pepe kwenda: IamBeijing@msichana.or.tz na nakala info@herabilityfoundation.co.tz

Maombi pia yanaweza kuwasilishwa moja kwa moja katika ofisi za Msichana Initiative
MIKOCHENI, MTAA WA TWIGA, NYUMBA NA .8 KINONDONI –DAR-ES-SALAM au
kutumwa kupitia S.L.P 12652

Mwisho wa kutuma maombi ni Februari 15, 2020 saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kwa maswali au maelezo yoyote ya ziada usisite kuwasiliana nasi kupitia barua
pepe: Info@msichana.or.tz au simu namba: 022-277-4100
Tafadhali kumbuka kwamba tutawasiliana na wale tu watakaochaguliwa